Misitu ni rasilimali
by Consolatha Nicholaus Sileyo
Ninalo langu swali,
nijibuni kwakujali,
itulie yangu hali,
si lazima ni hiyari.
Suali lenyewe hili,
kwazo hizi amali,
yupi miliki halali,
Wao au serikali.
nikianza na misitu,
Ipo karibu na watu,
huko ni katazo katu,
hata iingie kiatu.
wamiliki ndio wao,
karibu na miti yao,
walipewa babu zao,
wairithi iwe yao.
Sasa muwaingilie,
mahali mupavamie,
muwambie kwenu nyie
haki wasiwaelewe.
lengo ni kusimamia,
siyo jingine mwania,
mana walisimamia,
tangu wamewaambia.
Mengi umenikumbusha
Ukweli si kunichosha,
Ukweli nawapasha,
Ni ukweli usokisha.
Ile misitu na maji,
Na mito kama rufiji,
Ni nyenzo uzaliji,
O' mali kwa wapigaji.
Udongo pia nishati,
Ya jua sio ya shoti,
Umeme ulo simati,
Ni busara tukaketi.
langu moja swali,
Nauliza ukweli,
Na zitumike akili,
Kwa jibu li'lokamili.
Misitu ile kukata,
Tena makazi kupata,
Siyo sababu ukata,
Kosa liko wapi?
About
Iām a student, I study archaeology and geography.
Follow Consolatha on Twitter @consolatha26